Kongamano la Shirikisho la Machinga Tanzania limefanyika Mkoani Rukwa kwa kumpongeza Mhe Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga Kiasi cha Fedha Shilingi Bilioni 18.5 kwa ajili ya kuwakopesha Wajasiriamali(Machinga) Nchi nzima.
Kongamano hilo limehusisha makundi mbalimbali yakiwemo Boda boda,Bajaji pamoja na Wajasiriamali wa Mazao mbalimbali ,awali akitoa Hotuba kwa niaba ya umoja wa Machinga na Wajasiriamali Mkoa wa Rukwa Thobias Mgala ambaye ni Katibu Umoja wa Umoja huo ametoa Pongezi kwa Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akiunga juhudi kwa Taasisi zisiszo za Kiserikali ikiwa ni pamoja na Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania amabao wamekuwa ni wanufaika katika Mikopo mbalimbali inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita na kusema kuwa Kiasi cha kilichotengwa Nchini zinaenda kuwainua Kiuchumi , na kukuza mnyororo wa thamani .
Mgeni Rasmi katika Kongamano hilo Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Charles Makongoro Nyerere ambapo amewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe.Nyakia Ally Chirukile ameleza kuwa tayari Serikali Mkoani Rukwa imesaini Mkataba wa Soko jingine la Kimataifa litakalojengwa Mtaa wa Kanondo Manispaa ya Sumbawanga ili kuwewezesha Wajasiriamali kupelekza Mazao yao na kufanya kazi katika Mazingira bora na ya Kisasa zaidi.
Katika kuhakikisha juhudi zinazofanyika na Serikali baadhi ya Wananchi wapongeza na kutoa maoni ambayo matarajio yao ni kuona vikwazo vinaondoshwa katika upatikanaji wa Mikopo inayotloewa na Serikali katika kuwasaidia Wajasiriamali.