Wizara ya Maji Nishati na Madini ikishirikiana na Shirika la USAID imeandaa mikakati maalum ya matumizi ya Nishati mbadala hasa Umeme wa Jua, kwa Watumiaji wakiwemo Wawkezaji wa Hoteli Nchini.
Huyo ni Said Omar Abdalla, Mkuu wa Divisheni ya maendeleo ya Nishati kutoka idara ya Nishati na Madini Zanzibar akimuakilisha Mkurugenzi wa Idara hiyo Said Hadi Mdungi amesema kuwepo kwa matumizi ya Nishati hiyo kutaondoa matatizo ya Umeme mdogo, hasa kwa Wafanyabiashara hao wenye mahitaji makubwa zaidi katika sguhuli zao.
Mkurugenzi ukuaji wa Uchumi Tanzania wa USAID, Plato Hieronimus amesema USAID inaunga Mkono Sekta ya Utalii Zanzibar imeahidi itahakikisha upatikanaji wa nishati hiyo nchini inaongezeka.
Fredy msafiri miongoni mwa Wadau Walioshiriki katika Warsha hiyo, amesema Nishati mbadala ni nafuu itakayowapunguzia gharama wawekezaji na Wananchi wa Zanzibar.