MFUMO WA KIELEKRONI MAHAKAMANI WARAHISISHA UENDESHAJI WA KESI

KHAMIS RAMADHANI ABDALLA
English

Jaji Mkuu Wa Zanzibar, Khamis Ramadhani Abdalla Amesema Kuwepo Kwa Mfumo Wa Uendeshaji Wa Mashauri Kwa Njia Ya Kielektroniki Kumerahisisha Usikilizaji Wa Kesi, Na Kuchangia Upatikanaji Wa Haki Kwa Haraka.

Akizindua Mfumo Wa Majaribio Wa Uendeshaji Wa Mashauri Kwa Njia Ya Kielektroniki Huko Verde Amesema Lengo La Kuanzisha Mfumo Huo Ni Kuongeza Ufanisi Na Uwajibikaji Katika Mahkama Pamoja Na Kuondosha Urasimu Wa Haki Kwa Wananchi.

Mratibu Wa Ujenzi Wa Mradi Wa Mfumo Wa Uendeshaji Wa Mashauri Kwa Njia Ya Kielektroniki Jaji Ibrahim Mzee Amesema Mradi Huo Umelenga Kutoa Huduma Bora Kwa Njia Ya Kielectroni Za Mahkama Na Kuachana Na Mfumo Wa Zamani Wa Karatasi

Msimamizi Wa Ujenzi Wa Mradi Wa Mfumo Wa Uendeshaji Wa Mashauri Khatibu Pandu Buyu Amesema Mpka Mfumo Upo Katika Hatua Nzuri Na Unatarajia Kumalizika Mwezi Ujao Kwa Lengo La Kuanza Kufanya Kazi Zake Ipasavyo. 

Washiriki Wa Mfumo Huo Wa Majaribio Wamesema Kukamilika Kwa Mfumo Huo Utasaidia Upatikaji Wa Haki Kwa Njia Ya Kielectroni Na Kuondosha Urasimu Ndani Ya Mahkama Za Hapa Nchini. 

 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.