SHERIA BORA YA HABARI KUIMARISHA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI

MWENYEKITI ZPC

Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar ZAMECO imeadhimia kufuatilia kwa karibu zaidi Sheria mpya za habari ambazo Zina mapungufu yanayoathiri ukusanyaji na upokeaji habari

Akizungumza katika tathimini ya maadhimisho ya Siku ya uhuru wa Vyombo vya Habari Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Zanzibar ZPC Abdallah Mfaume amesema kuendelea kuwepo Sheria zisizo sahihi ni kuzorotesha kasi ya usatawi wa Demokrasia

Wadau na Wanaharakati wa Masuala ya habari wameshauri umuhimu wa kuendelea kuandika habari ,Makala na Vipindi vitakavyosaidia Mageuzi ya kisera na kisheria ili Waandishi kuendelea kufanya kazi zao kwa Uhuru

Akifunga Mjadala huo Mwandishi wa Habari Mwandamizi Salim Said Salim amesema wanapoomba uhuru wa Vyombo vya Habari wanadai haki yao hivyo Serikali ione umuhimu wa suala hilo kwa kuharakisha Sheria hiyo

Kamati hiyo ya Wataalamunwa masuala ya Habari imehusisha chama cha waandishi wa habari wanawake Tamwa Zanzibar,Jumuiya ya Waandishi wa Habari za Maendeleo Zanzibar wahamaza,Klabu Waandishi Habari Zanzibar ZPC na Baraza la Habari Tanzania MCT

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.