Kuwepo kwa huduma bora za Afya kutawasaidia Wananchi kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Hayo yameelezwa na Wakaazi wa Chaani katika Siku ya Matibabu katika Kijiji hicho yalioandaliwa na Taasisi ya Direct Aid Wananchi hao wamesema kuimarika kwa Matibabu ya Kiafya Mwilini kutasaidia kufanya kazi zao kwa wakati hivyo wameishukuru Taasisi hiyo na kukiomba kuwa suala hilo liwe la muendelezo.
Daktari Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini 'a' Dkt.Himidi Juma Said amesema kuna Idadi kubwa ya Wagonjwa ambao wanahitaji huduma bora hivyo wamejipanga kuhakikisha Wilaya ya Kaskazini 'a' Wanaweka Siku Maaluma kwa kila Mwezi ili kuwapa fursa Wanajamii kupata huduma hizo hivyo amewataka wadau wa afya kuwapa ushirikiano ili kufikia lengo.
Afisa kutoka Taasisi ya Direct Aid Shabani Ali Nahoda amesema Taasisi hiyo imejipanga kushirikiana na Serikali kwa kuwasaidia Wanajamii katika huduma mbalimbali ikiwemo Afya hivyo ametoa wito kwa wakaazi wa Kijiji hicho kushirikiana kwa pamoja.