WAZIRI TABIA AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KATIKA KUPIGA VITA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA

Waziri Tabia

     Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema usafirishaji na usambazaji wa dawa za kulevya umekuwa ni tatizo nchini na duniani kwa ujumla.

     Ameyasema hayo katika bonanza la kuelekea maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya lililofanyika katika viwanja vya Maisara Mjini Unguja.

     Amesema tafiti zinaonyesha kuwa Zanzibar inakisiwa kuwa na watumiaji wa dawa za kulevya zaidi ya elfu sita wakiwemo vijana, hivyo kutokana na tafiti hizo kila mmoja anawajibu wa kupambana katika kutokomeza uingizaji, usambazaji na utumiaji wa dawa hizo.

     Naye Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kudhitibi na Kupambana na Dawa za Kulevya Zanzibar Burhani Zubeir Nassor, ameeleza kuwa haifurahishi kuona baadhi ya watoto na vijana waliopo katika skuli za Msingi, Sekondari na Vyuo wamejiingiza katika matumizi ya biashara ya dawa za kulevya hivyo kunapaswa kutumika kila mbinu kuwatoa katika matumizi ya dawa hizo.

     Awali akitoa ushuhuda Ali Shau Ismail amesema matumizi ya dawa za kulevya yanaondosha thamani ya mtu katika jamii hivyo ni vyema kwa vijana kuachana na matumizi hayo ambayo yanaondosha heshima katika jamii.

     Maadhimisho ya siku ya kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya kitaifa yatafanyika Juni 26 Kisiwani Pemba na kauli mbiu ya mwaka huu ni "ushahidi upo wazi wekeza katika kuzuia matumizi na usambazaji wa dawa za kulevya".

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.