MH.HEMED AMNADI MGOMBE UBUNGE JIMBO LA KWAHANI KWA TIKETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

MAKAMO WA PILI NA MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KWAHANI

     Chama cha Mapinduzi CCM kimesema kitaendelea kutekeleza vyema ilani ya Chama kwa kuimarisha Miradi mbalimbali ya maendeleo Nchini.

    Mjumbe wa Kamati Kuu CCM ambae pia ni Makamo wa Pili wa Raisi wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdullah akizungumza katika Ufungaji wa Kampeni za Jimbo la Kwahani pamoja na Kumnadi Mgombea wa Jimbo hilo kwa Tiketi ya CCM amesema Viongozi wamekuwa wakichukua juhudi za kuimarisha Sekta muhimu za Kijamii ikiwemo kuimarisha Sekta ya Afya, Elimu Maji safi na salama na miundombinu rafiki ya ukuaji wa kiuchumi Nchini.

    Aidha Mhe.Hemedi ameongeza kuwa  ili kufanikisha ushindi wa Chama hicho ni lazima Wananchi kujitokeza kwawingi katika vituo vya kupigia kura huku akiwasisitiza kuimarisha ulinzi na usalama wakati wa Kupiga Kura na watakapomaliza kupiga Kura hizo.

    Mgombea wa Ubunge Chama cha Mapinduzi CCM Khamis Yussuf Mussa Pele ameahidi kutekeleza yale yote yaliokuwemo katika ilani ya CCM na kuwataka Wananchi kuendelea kumuunga Mkono ikiwemo kujitokeza kwa wingi katika Kupiga Kura.

    Mwenyekiti wa Mkoa Mjini Talib Ali Talib amesema CCM hairidhiiswi na tabia ya baadhi ya Vyama Pinzani kuwatolea Maneno yasio faa Viongozi waliokuwepo Madarakani huku akisisitiza kuwa wataendelea kusimamia amani umoja na ushirikiano .

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.