Wananchi wa Kwarara Kidutani wamesema upatikanaji wa Maji safi na salama utasidia kwa kiasi kikubwa kufikia maendeleo ya Wananchi kwa kuwapunguzia usumbufu waliokua nao.
Moja kati ya changamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili ni upatikanaji wa huduma ya Maji safi na salama ndani ya Kijiji hicho jambo ambako lilikiwa likirejesha nyuma juhudi zao za kujikomboa Kiuchumi.
Wakizungunza na ZBC mara baada yauzinduzi wa Kisima cha Maji safi na Salama kilichochimbwa kwa ufadhili wa Jumuiya ya Falah Islamic Foundation Wananchi hao wamesema hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kufia maendeleo kama Serikali kupitia ilani ya chama cha mapinduzi ilivyoahidi wakati wa Kapeni za uchaguzi wa Mwaka 2020.
Akizindua kisima hicho kilichogharimu zaidi ya Shilingi Milioni kumi ambacho kitahudumia zaidi ya Wanchi 300 wa Kijiji hicho Mrajis wa Jumuiya zisizo za Serikali kutoka wizara ya Nchi Afisi ya rais tawala za Mikoa na idara maalum za SMZ Ahmed Khalid Abadallah amesifu hatua ya Jumuiya ya Falah kwa kuona ukubwa wa tatizo la upatikanaji wa maji ndani ya Kijiji hicho na kufanya haraka kulitatu.
Ali Hashim ni Muwakilishi wa Jumuiya ya Falah Islamic Foundation akizungumza katika Hafla ya Unduzi wa Kisima hicho amesema Jumuiya hiyo itaendelea kishirikiana na Serikali katika kutatua changamoto zinazoikabali Jamii ikiwemo upatikanaji wa Maji Safi na salama.
Huu ni mradi wa kwanza kutekezwa na Jumuiya ya Falah Islamic Foundation kwa hapa Zanzibar tokea kusajiliwa kwake na umeuchukua Takriban Wiki Mbili hadi kukamilika.