MAAFISA UTUMISHI WATAKIWA KUTHAMINI MASLAHI YA WATUMISHI WA UMMA

WAZIRI JAFO

    Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ambae pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Seleman Jafo amewataka Maafisa Utumishi kuhakikisha wanajali na kuthamini maslahi ya Watumishi wa Umma kwani kufanya hivyo kutasaidia kuongeza ari na ufanisi wanapokua katika Majukumu yao.

      Akizungumza katika Hafla fupi ya kuwaaga Watumishi Wastaafu katika Kada ya Afya Wilayani Kisarawe, Dkt. Jafo amesema tabia ya baadhi ya Maafisa Utumishi na Wakuu wa Idara kujiona kama Miungu Watu pamoja na kutowapandisha Wauguzi Madaraja pamoja na kutopandisha Kiwango cha Mishahara kwa Muda Mrefu imekua ndio sababu inayochangia kushusha molari ya Watumishi kufanya kazi kwa weledi na uadilifu.

    Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Dk. Risas Rajabu akatumia fursa hiyo kuwatia moyo ikiwemo kuwaeleza umuhimu wa Wauguzi katika Sekta ya Aafya huku akiwataka kuendelea kufanya kazi kwa Moyo wao wa dhati ili kuwahudumia Wananchi wanaofika katika Vituo vyao kwaajili ya kupatiwa Matibabu.

    Akisoma Risala kwa Mgeni Rasmi Afisa Muuguzi Msaidizi Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe Zubeda Gumbo amezitaja kadhia wanazokumbana nazo ambazo ni Wauguzi kutopandishwa Madaraja kwa muda mrefu, upungufu wa Wafanyakazi pamoja na upungufu wa Nyumba za Wauguzi karibu na Vituo vyao vya Kazi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.