TIMU YA TANZANIA YATINGA FAINALI YA 'ASFC 2024'

Tanzania Timu

     Timu ya Tanzania ya wavulana imefuzu hatua ya fainali ya mashindano ya Mabingwa kwa Shule za Afrika (ASFC) kwa mwaka 2024 yanayofanyika visiwani Zanzibar.

   Wamefuzu baada ya kupata ushindi dhidi ya Benin kwa magoli 2-0 katika mchezo uliochezwa Mei 23,2024.

     Fainali itachezwa dhidi ya Guinea ambayo imepata ushindi kwa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya Senegal baada ya kutoa suluhu kwa dakika 90.

     Fainali hio itachezwa katika Uwanja wa New Amaan Complex-Zanzibar, Mei 24,2024.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.