Mkaguzi kata ya Mnyanjani Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/IVil, Faharia Massala akifuatilia Mienendo ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kwanjeka Wilaya ya Tanga jiji, Mkoa wa Tanga amewaomba walimu kuhakikisha wanafuatilia na kupata taarifa za wanafunzi hao ili kukomesha vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa Watoto hao.
Mkaguzi huyo ametoa rai hiyo shuleni hapo ambapo amebainisha kuwa watoto hao wanapaswa kupewa malezi na kufuatiliwa kwa karibu kutokana na vitendo vya baadhi ya watu wasio na maadili kuwafanyia watoto ukatili.
Ameongeza kuwa amekuwa na utaratibu wa kufuatilia Usalama wa Watoto mashuleni ambapo amewataka walimu kuhakikisha kila mwanafunzi anafuatiliwa kwa Karibu ili kubaini kama watoto hao wamefanyiwa vitendo viovu.
Vilevile alisisitiza kuwa licha kufanya hivyo kwa minajili ya Usalama wa watoto itasaidia kumaliza changamoto ya vitendo vya ukatili na utoro mashuleni.
Pia aliwataka walimu na wanafunzi Shuleni hapo kufahamu kuwa amepewa dhamana ya kuisimamia na kuhakikisha wananchi wa kata hiyo wanakuwa salama ambapo hatopenda kuona vitendo vya ukatili vinakuwepo katika kata yake.