WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATAKA MAZINGIRA WEZESHI KWA VYOMBO VYA HABARI.

WAZIRI MKUU TANZANIA

 Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa, amezitaka Mamlaka zinazosimamia Sekta ya Habari Nchini, kuimarisha Mazingira wezeshi kwa Waandishi wa Habari za Mitandaoni, ili kufikia uchumi wa Kidijitali.

 akizungumza katika Kongamano la Wamiliki wa Vyombo vya Habari za Mtandaoni, Mhe Kassim amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Wadau wa habari za Mitandao ya Kijamii na Vyombo vya Habari, ili kuharakisha ukuaji wa maendeleo Nchini.

Aidha Mhe Majaaliwa amesema Serikali inaendelea  kuimarisha Sheria na miongozo inayosimamia sekta ya habari, ili kuwawezesha waandishi wa habari kufanya kazi zao kwa uhuru na kuzingatia maadili, tamaduni na haki za watu wengine.

 waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe Nape Nnauye, amewahimiza waandishi wa habari na wamiliki wa vyombo vya habari, vikiwamo vya Mtandaoni kufanyakazi kwa kuzingia maadili ya Taaluma ya kazi zao.

Kwa Miaka Mitatu ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Sekta ya Habari Nchini imeendelea kuimarika na Uhuru wake, kwa kuondoshwa Shinikizo la vikwazo vya Sheria kandamizi ambapo

Kongamano hilo limefanyika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, na limeandaliwa na Jumuiya ya wamiliki wa Vyombo hivyo vya Mitandaoni Jumikita kwa Ushirikiano na Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu  Tanzania Tahliso.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.