WANANCHI WA KIPATO CHA CHINI KUNUFAIKA NA NYUMBA ZA GHARAMA NAFUU

KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI NA MAENDELEO YA MAKAAZI.

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Khadija Khamis Rajab amesema Wizara ina Mpango wa Ujenzi wa Nyumba za gharama Nafuu na Biashara ambazo zimewalenga zaidi WANANCHI wa kipato cha chini ili kukidhi mahitaji.

Akizungumza katika muendelezo wa Ziara zake na kuangalia maeneo ambayo Serikali inatarajia kujenga Nyumba za gharama nafuu na Biashara katika maeneo ya Kibele, Dunga, Mwera, Kitogani na Chumbuni.

 Mkoa wa Kusini Unguja, Katibu Mkuu huyo amefahamisha kuwa lengo hasa ni kuangalia uhalali na umiliki ili Wizara iweze kuja na mpango madhubuti wa Ujenzi huo.

Mkurugenzi Mkuu Shirika la Nyumba Zanzibar Mwanaisha Ali Saidi amesema Shirika na Mkuregenzi idara ya maendeleo ya Makaazi Hannat Bakar Hamad wamesema lengo ni kuona Wananchi hasa wa kipato cha chini wananufaika na Ujenzi wa Nyumba za gharama nafuu.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.