Zaidi ya Magunia 80 na Unga wa Makonyo yamekamatwa katika harakati za kusafirishwa kwenda nje ya Nchi kinyume na taratibu katika Shehia ya Msuka Wilaya ya Micheweni.
Akizungumza Kitendo hicho cha uhujumu wa Uchumi Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib amewataka wafanya biashara kufuata taratibu kulingana na Vibali vyao wanavyoomba.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la biashara la Taifa Zanzibar ZSTC Soud Saidi Ali amesema Serikali haijatoa ruhusa kwa Wananchi kusafirishwa Bidhaa zinazotokana na karafu kwenda Nje ya Nchi..
Magunia hayo ni Mali ya Mfanyabiashara Abdalla Khalfan Mohd mwenye Kibali cha Kununua Makonyo na Unga wa Makonyo kwa ajili ya kutengeneza Mafuta lakini amekitumia kibali hicho kinyume na Sheria na tayari anashikiliwa na Vyombo vya Sheria .