MICHUANO YA CAF AFRIKA SCHOOLS YAANZA RASMI ZANZIBAR

MICHEZO

      Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe.Tabia Maulid Mwita amesema Serkali inathamini juhudi za TFF na ZFF katika kufanikisha Mashindano ya Kimataifa kufanyika Zanzibar.

    Waziri Tabia ametoa kauli hiyo, alipofungua Rasmi Mashindano ya Kimataifa ya CAF Afrika Schools kwa Wasichana na Wavulana yanayofanyika Uwanja wa New Amaan Complex.

    Amesema juhudi za Mashirikisho ya Mpira zimesaidia Zanzibar kuendelea kutajika Kimataifa kwani Mashindano hayo yamekuwa Chachu ya Utalii wa Kimichezo Nchini.

     Nyota wa Zamani wa Arsenal,Manchester City na Real Madrid na Gwiji wa Timu ya Taifa Togo, Emmanuel Adebayor amesema Mashindano kama hayo hukuza Vipaji vya Vijana na kufurahia ndoto zao.

    Katika Ufunguzi wa Mashindano hayo, Timu ya Vijana chini ya Umri wa Miaka 14 ya Tanzania wametoka Sare ya Sifuri kwa Sifuri dhidi Senegali huku kwa upande wa Wanawake wakishinda bao moja kwa Sifuri dhidi ya Morocco, Afrika Kusini Wanaume wameshinda Bao 3-0 Dhidi ya Libya huku kwa Wanawake wakitoka Sare ya bao 1-1 dhidi ya Uganda, huku Timu ya Guinea Wanaume wameshinda bao 2-1 dhidi ya Benin huku Timu ya Togo wakitoka Sare ya Sifuri kwa Sifuri dhidi ya Gambia.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.