MWENGE WA UHURU KUTEMBELEA ZAIDI YA MIRADI 23 KATIKA MKOA WA MJINI MAGHARIBI

Makabidhiano Mwenge

     Jumla ya miradi 23 ya zaidi ya Billion 5 inatarajiwa kutembelewa na Mwenge wa Kitaifa wa Uhuru 2024 kwa Mkoa wa Mjini Magharibi.

    Akizungumza katika mapokezi ya Mwenge huo huko Uwanja wa Ndege Zanzibar Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Idrissa Kitwana Mustafa amesema mbio za Mwenge wa uhuru, Mkoani humo zitahusisha kilomita 104 na kutembelea miradi 23 ya maendeleo.

     Awali akitoa taarifa fupi ya Mkoa wake wakati akiukabidhi mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib amesema Mkoa wake uliupokea vyema Mwenge wa Uhuru kwa kuitahmini falsafa yake ambayo imeleta maendeleo chanya kwa Taifa.

    Amesema Mbio za Mwenge wa uhuru zimehusisha kilomita 459 na kutembelea Miradi yenye thamini ya Bilion 5.

      Naye Kiongozi wa Mwenge wa uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Eliakimu Mzava ameushukuru uongozi na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa mashirikino mema uliyowapatia.

      Aidha amewaomba Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa Mjini Magharibi kuwapokea na kuwapatia mashirikiano ili lengo la matembezi ya Mwenge huo yaweze kufikiwa kwa ufanisi.

     Mbio za Mwenge wa uhuru katika Mkoa wa Mjini Magharibi zinaaza Leo katika Wilaya ya Magharibi "B" kabla ya kuendelea katika Wilaya ya Mjini na Wilaya ya Magharib "A".

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.