NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KUWEKA MAZINGIRA RAFIKI YA ANGA

MAMLAKA YA ANGA

     Mkurugenzi Mkuu wa Anga Kenya Emile Ngunza Arao amesema mazingira raifiki yaliyowekwa katika Sekta hiyo Nchini humo, yamekusudia kuwawezesha Wwananchi kutumia Usafiri wa Anga.

     Akizungumza na Vyombo vya Habari baada ya kufunga Kongamano la Sita la Usafiri wa Anga la Jumuiya ya Afrika Mashariki, amesema moja ya uimarishaji huo ni kupunguza Bei ya Tiketi ili kuwezesha Wananchi wa Vipato vyote kumudu gharama za usafiri wa Anga.

     Mkurugenzi udhibiti uchumi Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA Daniel Malanga amesema ni muhimu kuwe na mpango endelevu wa ukaguzi wa mara kwa mara ili kuwa na usalama imara katika maeneo ya Anga.

    Mtendaji Mkuu Wakala wa Barabara Tanzania Mhandisi Mohamed Besta amesema wanashirikiana kwa asilimia kubwa katika ujenzi wa Viwanja vya Ndege ili kuhakikisha Usalama wa Anga unazidi kuimarika.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.