Viongozi wa Vyama vya Siasa wameomba kutekelezwa kwa vitendo falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kukuza Demokrasia Nchini kwa kuhakikisha hakuna mkwamo wa Kisaiasa kwa maslahi ya Wananchi.
Viongozi wa Vyama vya Siasa, Asasi za Kiraia na Viongozi wa Dini wanaokutana Zanzibar kwa Siku Mbili katika Kongamano la Demokrasia, wamesema iwapo falsafa hiyo inayohusisha mambo Manne yatafanyiwa kazi yakiwemo ya maridhiano, ustahamilivu na mageuzi ya Demokrasia, itawezesha kufikiwa maridhiano ya Kisiasa Tanzania na kukuza ustawi wa maendeleo.
Afisa Mtendaji wa Shirika la Centre for Strategic Litigation, (CSL) linaloshirikiana na Taasisi nyengine kuandaa Kongamano hilo Deus Valentine Rweyemamu, amesema ni busara kuwakutanisha Viongozi wa Kisiasa muda huu ili kujadili masuala yanayohusu Demokrasia kabla Nchi haijaingia katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka huu pamoja na Uchaguzi Mkuu Mwaka 2025.