Wazazi na walezi Mkoani Lindi wametakiwa kuitumia vyema mifumo iliyowekwa na Serikali katika kushughulikia migogoro na tofauti zinazojitokeza katika familia zao ambayo kwa kiasi kikubwa uchangia kuachana na kusababisha watoto kuathiriwa kwa kukosa malezi imara.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo katika maadhimisho ya siku ya Familia ambayo kwa ngazi ya Mkoa yamefanyika katika viwanja vya soko la majengo halmashauri ya Mtama Mkoani humo.
Ndemanga amesema Mifumo hiyo ni pamoja na madawati ya jinsia na Ofisi za ustawi wa jamii zilizopo kwenye kila halmashauri.
Ndemanga ametaka wazazi kunitumia siku hii kutafakari namna ya kuimarisha ubora wa familia ikiwemo kutafuta suluhu ya tofauti zao kwa njia zinazofaa ili zisiendee kuathiri malezi na makuzi ya watoto.
“Watoto wetu wakati wanaimba wamekuambia kwa lugha nyepesi sana kwamba tunapogombana baba anakuwa na lakwakwe na mama pia anakuwa na lakwakwe hakuna anauejihusisha na malezi tunawapa shida watoto,lakini kwa hapa Lindi tunautamaduni wetu,wazazi tunapofarakana na kuachana tunaacha jukumu la ulezi kwa babu na bibi na wazazi hawawajibiki tena’Alisema Ndemanga.
Awali,Akimuwakilisha Katibu Tawala Mkoa wa Lindi,Zuwena Omari,Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt Kheri Kagya ameweka wazi namna ambavyo migogoro ndani ya familia inavyoathiri watoto ambapo amesema katika kipindi cha mwaka 2023/2024 Mkoa wa Lindi unajumla ya Watoto 3797 walio katika mazingira magumu ambao wametokana na familia ambazo zinamigogoro na malezi yasiyofaa huku katika madawati ya jinsia na ustawi wa jamii kukiwa na mashauri ya migogoro ya familia 13796 ambayo kwa sehemu kubwa yanahusu wazazi waliotelekeza watoto na kutotoa matumizi.
Kwa upande wake Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Lindi Joyce Kitesho amesema Jeshi la Polisi wanayo kampeni ya ushirikishwaji wa jamii isemayo familia yangu haina muhalifu kwani uhalifu huwa unaanzia kwenye ngazi ya familia endapo wazazi hawatotimiza majukumu yao kikamilifu na akatumia nafasi hiyo kuwaomba wazazi kuwa walezi na sio watoa huduma.
Siku ya Familia Kimataifa Imeenda sambamba na kauli mbiu isemeyo tukubali tofauti zetu kwenye familia kuimarisha malezi ya watoto.