JESHI LA POLISI KUANZISHA MKAKATI WA KUKOMESHA VIJANA KUTEMBEA NA SILAHA ZA JADI IKIWEMO MAPANGA ILI KUONDOA UHALIFU.

KAMANDA WA PILISI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi limeanzisha Mkakati wa  maalum wa kutembelea Nyumba kwa Nyumba na kuhakikisha Vijana hawatembei na Silaha yoyote ya Jadi itakayosababisha kuhatarisha Usalama wa wananchi katika Jamii.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Kikao kilichowashirikisha Vikundi maalum vya Ulinzi Shirikishi na Masheha Washehia mbalimbali za Wilaya ya Magharibi B Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharib Sacp Richard Tadei Mchonvu ameseam wameanzisha Uperesheni hiyo kwa lengo la kuhakikisha uhalifu wa Vijana kutumia Silaha za Jadi ikiwemo Panga na Visu  ukomeshwe katika Jamii na kuwataka Wananchi kuishi bila ya wasiwasi. 

Kamanda Mhomvu amesema Uperesheni hiyo itakuwa endelevu na itawahusisha Masheha, Wakaguzi wa Shehia, Vikundi vya Ulinzi Shirikishi ambao ndio miongoni mwa Wananchi ambao ndio Wazazi wa Vijao hao na maeneo  yatakayoanzia Uperesheni hiyo ni Fuoni pamoja na Mwanakwerkwe kutokana na kukithiri kwa Vitendo vya Uhalifu huo.

Masheha wa Shehia mbalimbali za Wilaya ya Magharibi B wamesema Watashirikiana na Jeshi hilo ili kuhakikisha wanafanikiwa pamoja na kuwataka Wazazi kusimamia wajibu wao kwa Watoto na hata Wenza wao kuhakikisha Vitendo vya Uhalifu vimeondoka katika Shehi zao.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.