KAMISHENI YA UTALII ZANZIBAR NA TAASISI YA UTALII YA JEJU ZASAINI HATI YA USHIRIKIANO KATIKA KUKUZA UTALII

Kamisheni ya Utalii Zanzibar na Taasisi ya Utalii ya jeju

     Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZTC) na Taasisi ya Utalii ya Jeju (JTO) leo zimesaini Hati ya Maridhiano (MoU) ya kushirikiana katika kukuza utalii katika hafla fupi iliyofanyika katika kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.

     Hati hiyo imesainiwa na Bi. Hafsa Mbamba, Katibu Mtendaji wa ZTC na Bwana Koh Seung Chul, Afisa Mtendaji Mkuu wa JTO, na kushuhudiwa na Mheshimiwa Mudrik R.Soraga, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.

    Makubaliano hayo yatalenga katika kushirikiana kutangaza Utalii kati ya visiwa hivyo viwili pamoja na kupanga mikakati ya kukuza masoko, kubadilishana uzoefu na kutoa taarifa zinaweza kusaidia kujenga Utalii kwa visiwa hivyo viwili.

    Zanzibar na Jeju ni visiwa vyenye sifa zinazofanana haswa ukizingatia uchumi wake umejikita katika sekta ya utalii ambao unatunza mazingira, Shana ya Utalii endelevuu na kuwa wanachama wa Inter-Islands Tourism Policy Forum (ІТОР).

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.