WATOTO WATAKIWA KUPATIWA ELIMU BILA KUJALI JINSIA ZAO

Mradi Korea

     Shirika la Korea khfi linalosimamia Mradi wa kutengeneza Mazingira Rafiki kwa Mtoto wa Kike kuweza kumaliza masomo yake, limewataka Wazazi kuangalia umuhimu wa kuwapatia elimu Watoto bila kujali jinsi zao.

     Akizungumza na Wazazi wa Wanafunzi wa Skuli ya Mtule waliopatiwa Mafunzo ya Siku Nane ya Elimu ya Jinsia, Meneja Miradi wa khfi, Taewan Park, amesema elimu ya jinsia ni msingi wa kujenga Jamii jumuishi kwa Wanawake na Wanaume.

     Amesema Shirika lake kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, limeanza kutengeneza mazingira rafiki ya kujisomea kwa Wanafunzi hasa wa Kike, ambao wanakumbana na vikwazo vingi katika safari yao ya masomo.

     Nae Afisa Afya ya Uzazi, Ukimwi na Dawa za Kulevya, kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Riziki Mohamed Juma, amewataka Wazazi kuwa makini katika kuwasimamia Watoto na kuhakikisha lengo la kuwapatia Elimu linafanikiwa. 

    Akifunga Mafunzo hayo Afisa Elimu Wilaya Kusini Mussa Nahodha Makame, amesema Elimu ya Jinsia iliyotolewa imelenga kuweka mazingira bora ya kimaisha kwa Wanafunzi, Wazazi na Jamii kwa ujumla.

     Nao baadhi ya Washiriki  wamesema wamepata muongozo wa kuweza kuielimisha Jamii kuhusiana na kuweka usawa katika malezi, na kuhamasisha Wanawake kushiriki katika shughuli mbali mbali za maendeleo.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.