Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla yamesemwa hayo alipofungua mafunzo ya kuwaendeleza Wataalamu wa Usanifu, uhandisi na Wakadiriaji Majengo Tanzania huko Nyamanzi Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Amesema Serikali zote Mbili zimetoa kipaombele kwa Wataalamu wa Ujenzi na Makampuni ya ndani ya Nchi kupitia Wizara na Taasisi ambazo zimefanya juhudi za kuweka Sera, Sheria na Kanuni zenye Vigezo Rafiki ili kurahisisha Maombi ya kazi za Ujenzi Nchini.
Aidha Mhe Hemed amesema matumaini makubwa ya Serikali kuwa Mafunzo hayo yatasaidia kuonesha mbinu za kuhifadhi, kuitunza na kuiendeleza Miji ya Urithi ambayo inaongeza pato la Taifa huku akiwataka Washiriki kuitumia vyema nafasi waliyoipata ili kupata uwelewa na mbinu mbali mbali za Ujenzi.
Akiwasilisha Taarifa ya Wizara ya Ujenzi, Mawasiano na uchukuzi katibu Mkuu Wizara hiyo Dkt. Mngereza Mzee Miraji amesema kufanyika kwa Mafunzo haya kunatokana na ushirikiano kwa pande mbili za Muungano kwa lengo la kuhakikisha Nchin inakuwa na Wataalamu Wabobevu hasa katika masuala ya kutunza na kuimarisha Miji ya Urithi wa Dunia.
Nao Wenyeviti wa Bodi ya usajili Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Majengo kutoka Zanzibar na Tanzania Bara wamezishauri Serikali kuangalia Sheria na miongozo katika masuala ya Ujenzi ili kupunguza tatizo la kujengwa kwa Majengo yasiokidhi viwango na kuendelea kulitia hasara Taifa Siku hadi Siku.