Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Riziki Pembe amewasisitza Masheha Mkoa wa Kusini Unguja kuwaorodhesha Wazee wote ambao wameshafikia umri wa kupokea Pencheni Jamii ili waweze kunufaika na fursa na haki hiyo.
Akizungumza na Masheha hao amesema ni vyema kwa Masheha kuangalia Wazee ambao wana mkanganyiko wa vielelezo vya Vitambulisho kutumia njia mbadala kuhakikisha hawakosi haki yao hiyo kwa kisingizio chochote.
Benki ya Watu wa Zanzibar kupitia Muakilishi wake Naila Madai Ali ameomba Masheha kushiriki katika Vikao vya Pencheni Jamii wanaposajiliwa Wanachama wapya na kuwafahamisha Masheha mfumo unaotumika kulipwa Pencheni zao kwa njia ya Benki.
Wakati huo huo Waziri ameishukuru Polisi kusimamia Ulinzi na Usalama katika Mkoa huo na kuwezesha kupungua suala la Dawa ya kulevya na kuiomba kuharakisha majadala ya upelelezi wa kesi za udhalilishaji ili hatua za Kisheria zichukuliwe dhidi ya Watuhumiwa.
Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Mabaraza ya Watoto Zanzibar amewataka Masheha hao kuisaidia Wizara ya maendeleo ya Jamii kusimamia Mabaraza ya Watoto katika majukumu ya Ushirikishwaji wa kutoa maoni ykatika Ngazi za Shehia, Wilaya na Mikoa.
Nao baadhi ya Masheha wa Shehia malimbali za Mkoa huo wamemshukuru ziara hiyo ya Waziri kukutana nao na kuwahidi kuyafanyia kazi maelekezo aliyoyatoa.