Umoja wa Vyama vya Siasa Tanzania wamelaani baadhi ya Wanasiasa kutumia kauli za kuchafua Viongozi pamoja na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na badala yake wajenge umoja na mshikamano.
Akitoa Taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusiana na kauli za Makamo Mwenyekiti wa Chadema Tundu LIssu Mwenyekiti wa umoja huo Tanzania Mh Juma Ali Khatib amesema kuendelea kufanya hivyo ni kuutumia uhuru vibaya na kuwagawa Wananchi.
Kufuatia hali hiyo ameviomba Vyombo vya Ulinzi na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini kufanya uchunguzi wa kina kuhusiana na kauli hizo na kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria za Vyama vya Siasa ili kuendelea kuilinda Amani iliopo
Mwanaharakati wa haki za Binaadamu Ali Makame Issa amesema jukumu la kulinda Muungano ni la Watu wote hivyo hatua za Kibaguzi na kukebehi baadhi ya Makabila yaliyopo Nchini kunaweza kuwagawa Wananchi na kuathiri malengo ya kuasisi Muungano huo
Mwenyekiti NCCR Mageuzi Haji Ambar Khamis amesema Viongozi wa TANZANIA wamesimamia mambo muhimu katika Nchi ikiwemo kutoa uhuru katika masuala mbali mbali hivyo si vyema wanasiasa kuutumia vibaya uhuru huo
Jumla ya Vyama 11 vya Siasa Tanzania vimetoa kauli ya kulaani Wanasiasa wanaoyatumia vibaya majukwaa ya kisiasa vikiwemo NCCR Mageuzi,Tadea nra na Demokrasia makini