KITUO CHA KISASA CHA HUDUMA NA MATIBABU YA SARATANI KIMEZINDULIWA AGA KHAN HOSPITALI

SARATANI

     Naibu Waziri Mkuu ambae pia ni Waziri wa Nishati Dkt.Mashaka Doto Biteko amezindua Kituo cha Kisasa cha huduma na Matibabu ya Saratani katika Hospitali ya Aga-Khan Jijini Dar es salaam.

      Kuzinduliwa kwa Kituo hicho chenye hadhi ya Kimataifa ni Matokeo ya utekelezaji wa mradi mtambuka wa Saratani Tanzania wa Tccp.

     Akizungumza kwa Niaba ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan katika Hafla ya Uzinduzi wa Kituo hicho ambacho kinalenga kutoa msaada wa Asilimia 35 ya Wagonjwa wa Saratani ambao hawezi kumudu Matibabu Mh. Biteko amesema Serikali chini ya Raisi Samia itaendelea kushirikiana na Sekta binafsi katika kuboresha na kuimarisha mifumo ya utoaji wa huduma za afya Nchini Tanzania.

    Awali akimkaribisha Mhe.Biteko Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema tatizo la Ugonjwa wa Saratani hapa Nchini bado kubwa ambapo takribani Wagonjwa Efu 40 Wapya hugundulika kila Mwaka huku likisababisha vifo Elfu 27. na kusisiza kuwa ni vyema hatua zikachuliwa ili kudhibiti hali hiyo.

     Naibu Katibu Mkuu Afya Afisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dr.Grace Magembe amesema gharama za Matibabu ya Saratani ni za juu sana hivyo Jamii inapaswa kujikita zaidi katika kuzuia Magonjwa hayo.

    Ufunguzi wa Kituo cha Huduma ya Saratani katika Hospita ya Aga khan ya Jijini Dar es salaam utaimarisha huduma zinazotolewa na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na kupunguza muda wa kusubiri.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.