Mkoa wa Lindi umepokea Jumla ya Shilingi Tilioni 1.2 kwa ajili ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Elimu, Afya, Maji Umeme Barabara na huduma nyingine kwa Kipindi cha Mwezi March 2021 hadi March 2024
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack alipokuwa akizungumza na Wafanyakazi na Wananchi wakati wa maadhimisho ya Sherehe za Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika huko Wilayani Ruangwa
Amesema amesema Mafanikio hayo yametokana na utendaji kazi mzuri wa Watumishi huku akibainisha kuwa nchi zote zilizopiga hatua ya maendelea Ulimwenguni zilitokana na uwajibikaji na utendaji kazi kwa Watumishi katika Sekta mbalimbali
Amewapongeza Watumishi kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii licha ya matatizo mbalimbali huku Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Lindi Banarbas Esau akieleza namna chama kinavyolidhishwa na utendaji kazi wa Watumishi katika utekelezaji wa Ilani
Awali mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa Wilaya ya Ruangwa akaelezea umuhimu wa Siku hiyo ya Wafanyakazi