Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dr Khalid Salum Mohamed amesema mageuzi ya Kidigitali yanakwenda kwa kasi hivyo ni vyema matumizi ya Teknologia yakatumika ipasavyo.
Akifunga Mafunzo ya Wiki moja na Mashindano ya Tehama kwa Wasichana huko golden tulip Uwanja wa Ndege Dr Khalid amesema ni muhimu kuwepo na matokeo ya Teknologia hiyo kwani bado Teknologiajia ya utoaji wa huduma haijatumika ipasavyo.
Amesema Serikali zote Mbili zinatilia mkazo masuali ya Teknologia hiyo ambapo Vituo vya Tehama 11 vimejengwa katika wilaya zote za Unguja na Pemba.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dr Mngereza Mzee Miraji na Mkurugenzi Mkuu Tume ya Sayansi na Teknologia Dr Amous Nungu wamesema Mafunzo hayo yatakuwa na mwendelezo ili kuona malengo ya Tehama yanafikiwa.
Mtendaji Mkuu mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF), Justina Mashiba amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kwa Watoto wakike kutokana na kuwa na Mwamko mdogo.