MAMA LISHE PEMBA WAKABIDHIWA MITUNGI YA GESI

DK.FADHILA ABDALLAH HASSAN

Afisa Mdhamin Wizara ya kazi uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Dk.Fadhila Abdallah Hassan amewataka Wanawake kubuni mbinu mbalimbali ambazo zitawasaidia katika kupiga hatua mbele za kimaendeleo ili waweze kufikia malengo waliyoyakusudia ya kujiinua kiuchumi.

Dr Fadhila amesema hayo huko Pujini wakati wa ugawaji wa vitendea kazi kwa

Wanawake wanao jishughulisha na Shughuli mbali mbali za Mama Lishe Kisiwani Pemba Vilivyotolewa kwa ushirikiano wa Cocacola ,Orxy gesi, Zbc pamoja na wakala wa uwezeshaji kiuchumi Zanzibar.

Amesema lengo la Serikali na Wadau ni kuhakikisha inamtoa Mwanamke katika uchumi mdogo na kumkuza katika uchumi wenye tija kwa kupunguza hali ya umaskini wa kipato cha Mtu mmoja mmoja pamoja na kuongeza kipato na uchumi wa Taifa

Kwa upande wake Mratib wa shirika la utangazaji Zanzibar Zbc Khamis Ali Khamis na Kaimu Mratib Wakala wa Wananchi kiuchumi Pemba Haji Mohd Haji wamesema Vifaa hivyo walivyopatiwa vitaweza kupunguza uharibifu wa Mazingira pamoja na kufanya biashara zao kwa unadhifu zaid na kuwataka kuvitunza ili viweze kudumu kwa muda mrefu.

Nae Afisa masuala ya umma na udhibiti Cocacola pia ni Mratib wa Mwanamke Shujaa

Maria kimwaga amesema Kampuni ya Cocacola kwanza iko karibu na Jamii na imeona Kuwa suala la kumuwezesha na kumuwahisha Mwanamke kiuchumi inapelekea Jamii yote Kuenuka Kiuchumi.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.