Maafisa Manunuzi wa Taasisi za Serikali wameishauri Serikali kuandaa Programu za Mafunzo kwa Watendaji ili kufikia lengo la utowaji wa huduma bora.
Wakizungumza baada ya kumaliza Mafunzo ya Siku 5 juu ya kumtafuta Mshauri elekezi, wamesema kumekuwa na ongezeko la mahitaji ya huduma kutokana na mabadiliko ya Kidigitali, hivyo kupata mafunzo ni sehemu pekee ya kuimarisha utendaji.
Wakizungumzia kuhusiana na Mafunzo hayo wamesema yatawapa mabadiliko kwani hapo awali walikabiliwa na tatizo katika kupata mshauri elekezi sahihi.
Wamesema hali hiyo ilikuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi hasa katika eneo la mikataba hali iliyosababisha miradi kutokuwa na viwango.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Manunuzi Zanzibar Othman Juma Othman, amesema matarajio yao ni kupunguza asilimia kubwa ya malalamiko kuhusiana na na miradi kwa kupata washauri wenye uwezo na sifa
Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na mamlaka ya manunuzi na uondowaji mali za umma, washiriki walikabidhiwa vyeti vya kukamilisha mafunzo hayo.