Mratibu wa Tasaf Wilaya ya Ukerewe Jenitha Byagalama amesema Ujenzi wa Bweni na Bwalo la Chakula kwa pamoja umegharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 300 chini ya ufadhili wa Nchi zinazozalisha Mafuta Duniani.
Aidha ya Wanafunzi katika Kijiji cha Bukondo Wilaya ya Ukerewe kuvuka kwa Mitumbwi itapungua na usafiri wa Mitumbwi kwa Wanafunzi wanaotoka Kijiji cha Busumba aidha inayosababisha baadhi yao kukatisha masomo itaisha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe Emmanuel Shelembi amesema Kipaumbele cha Halmashauri hiyo ni kuendelea kuimarisha mazingira bora ya Wanafunzi kujifunzia.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Josephat Mazula akizindua na kukabidhi miradi huo ameitaka Jamii kulinda Miundombinu ya Mradi ili idumu na kutoa huduma ipasavyo.
Miradi iliyokabidhiwa kwa Jamii imetekelezwa kwa dhana ya uwazi, ukweli, ushirikishwaji na uwajibikaji, miradi iliyohitaji nguvu kazi jamii imechangia kwa asilimia 10 ya Fedha iliyotolewa na Mfadhili.