VIFAA VYA KUSHUSHIA MAKONTENA VYAWASILI BANDARI YA MALINDI

Shirika la Bandari

    Shirika la Bandari Zanzibar limesema tayari wameshaanza kutatua matatizo yanayolikabili hasa kwenye sehemu ya kushusha mizigo.

    Akizungumza baada ya kupokea Vifaa vipya vya kubebea mizigo huko Malindi Mkurugenzi wa Shirika la Bandari Zanzibar Akif Khamis amesema Mashine hizo zitawezesha kutatua matatizo yanayolikabili Shirika hasa kwenye sehemu ya kuchusha mizigo.

     Amesema Vifaa hivyo vina uwezo mkubwa wa kushusha Makontena katika muda mdogo zaidi ukilinganisha na vilivyopo sasa.

     Aidha Mkurugenzi Akifu amesema katika hatua nyengine Shirika la Bandari litawekaa Taa maalum kwenye Maeneo ya kushushia Makontena zitazowawezesha Wafanyakazi kufahamu utekelezaji wa kazi katika Eneo hilo.

     Meneja Mkuu wa Kampuni ya Zanzibar Multipurpose Terminal, Niclolas Escalin amesema kuwasili kwa Vifaa hivyo kutaongeza ufanisi katika utendaji wa kazi za kila siku.

     Zaidi ya Shilingi Bilion Mbili Nukta Nane zimetumika kununulia Vifaa hivyo.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.