Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema bado haiko tayari kuwa na utaratibu wa kutoa Uraia Pacha badala yake iko katika hatua za Mwisho kukamilisha utoaji wa Hadhi maalum kwa Raia wa Nchi nyingine wenye Asili ya Tanzania ili kuchangia ipasavyo katika Maendeleo ya Taifa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafaniko ya Wizara hiyo katika kipindi cha Miaka 60 ya Muungano Tanganyika na Zanzibar.
Aidha amesema Serikali ya Tanzania imefanikiwa kuimarisha Ushirikiano na Mataifa mengine katika Nyanja mbalimbali ikiwemo katika Maeneo ya Kibiashara .
stories
standard