Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt.Khalid Salum Mohammed amewataka Wadau wa Mkutano wa Kikanda juu ya usalama wa Vivuko Afrika kutoka na mkakati ambao utasaidia kuweka hali ya usalama wa vyombo vidogo vidogo vya Baharini, Ziwani na Mtoni ili kuweza kupunguza ajali zinazotokana na Vyombo hivyo katika Bara la Afrika.
Waziri Khalid ameyasema hayo wakati walipokuwa akifungua Mkutano huo Jijini Dar- es sallam amesema imeonekana kuwa kuna ajali nyingi zinatokea katika Vyombo hivyo ambazo husababisha maafaa makubwa ikiwemo Vifo, Watu kurejuhiwa pamoja na upotevu mali .
Amesema ipo haja ya kuwajengea uwezo Manahodha wanaoondesha Vyombo hivyo ili kujua njia gani wanaweza kupita na namana ya kutumia vizuri Taarifa za Hali ya Hewa.
Amesema ili kukabiliana na Ajali hizo kwa upande wa Zanzibar inakusudia kuweka rada ambayo itafuatilia Vyombo ambavyo vitakuwa vinafanya Safari zake kwa njia ya Baharini.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Azam Marine Abubakari Azizi Salum amesema Mkutano huo unatija kubwa katika kazi zao hasa kwa upande wa usalama na Biashara.