Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuanza Ziara ya Kiserikali Nchini Uturuki ikiwa ni hatua ya kuendeleza Ushirikiano wa Kidiplomasia na Kiuchumi baina ya Tanzania na Uturuki.
Akizunguzia Ziara hiyo Waziri wa mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki Mhe Januari Makamba amesema Rais Samia atawasili nchini Uturuki tarehe 17 kufuatia Mwaliko wa Rais wa Nchi hiyo Recep Erdogan ambapo pamoja na mambo mengine Rais Samia akiwa Nchini Turuki atafanya mazungumzo na Mwenyeji wake mazungumzo yanayolenga kuanzisha maeneo mapya ya kiushirikiano.
Aidha akiwa Nchini Uturuki Rais Samia atakwenda Istambul Jiji kubwa la Kibiashara ambako atahudhuria Kongamano la Kibiashara na kupata fursa ya kukutana na Wafanyabiashara 15 wenye Makampuni makubwa Nchini humo.