Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekusudia kuimarisha Sekta ya Elimu kwa Unguja na Pemba
Akizungumza hayo katika Ziara ya kuangalia maendeleo ya Mradi wa Skuli za Sekondari zinazojengwa Mfenesini na Gamba Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh Leila Muhamed Mussa ameasema kuwa Skuli zinazojenga zitaweza kuleta Mageuzzi makubwa ya Elimu.
Aidha amesema kuwa kati ya mageuzi hayo ni kuaanzisha Michipuo kwa wingi kwa kila Wilaya hivyo amewataka Wakandarasi hao kuharakisha zaidi ili kuweza kumaliza kwa wakati kwa mujibu wa makubaliano yao.
Hata hiyo amewapongeza Wakandarasi wa Mfenesini kwa kupiga hatua kubwa licha ya matatizo madogo madogo wanayoyapayta.
Kwa upande wa Gamba Mh Leila hakuridhishwa na maendeleo ya Ujenzi wa Gamba amemuagiza Katibu Mkuu wa Elimu na mafunzo ya Amali afuate taratibu za kimkataba za kuhakikisha Mkandarasi huo haaongezewi mda
Naye Mbarouk Salum msaidizi wa Injinia ameahidi kuwa tatizo lilowasaababissha hata kudhorota kwa Ujenzi ni kipindi cha Mvua , hivyo ameahidi kuwa Watafanyakazi kwa Bidii ili kufikia hali nzuri.