Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Al-haj Dkt Hussein Ali Mwinyi amejumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika ibada ya Sala ya Eid Fitri katika Msikiti wa Jamiiu Zinjibar Mazizini Zanzibar.
Akitoa Khutba ya Eid El fitri Khatib wa Sala hiyo Sheikh Abdulkarim Said Abdul amewahimiza Waumini wa dini ya Kiislam kuendeleza huruma, upole kama funzo linalotokana na Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
Amesisitiza umoja na mshikamano baina ya Waislam ili Nchi iweze kupata maendeleo zaidi.
Viongozi mbali mbali wa Serikali wamehudhuria akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Al- haj Hemed Suleiman Abdullah, Waziri wa Katiba Sheria Utumishi wa Umma na Utawala bora Mh Haroun Ali Suleiman Mufti Mkuu wa Zanzibar Shekh Saleh Omar Kaabi na Mashekh wa Baraza la Maulamaa .