SERIKALI KUENDELEA KUWAWEZESHA WANANCHI KIUCHUMI

Ugawaji wa Gesi

    Serikali imesema itaendelea kutoa msaada kwa Wanchi ili kuwawezesha kiuchumi.

     Akizungumza katika Makabidhiyano ya Gesi  huko Raha Leo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi , Uchumi na  Uwekezaji Mhe Sharif Ali Sharif amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuwawezesha Wananchi kujikimu kimaisha na kupunguza Matumizi ya Makaa na kuni ili kutunza mazingira na kuwa na Afya Njema. 

    Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe Tabia Maulid Mwita amesema lengo ni kusaidia Wanawake Wajasiriamali wa Mkoa wa Mjini ili kujikwamua kimaisha na kuwataka Wajasiriamali kuwafichua wakwepa Kodi ili kuengeza Pato la Serikali .

     Meneja Mkuu wa Oryx Gas amesema Gesi waliyotoa itakuwa na mchango mkubwa katika kulinda mazingira na afya njema kwa Mtumiaji wa Gesi kwa kuepukana na Moshi unatokana na Kuni na Mkaa.

   Wajasiriamali waliopokea msaada huo wamesema wamefurahi sana kwa kupata Msaada huo na utawasaidia sana katika Biashara zao na kuahidi kuwa Mabalozi wa zuri kwa wengine kutokana na Elimu ya Kodi waliyoipata ili Mapato ya Serikali yasipotee.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.