Wakati huohuo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki katika Maziko ya Mbunge wa Jimbo la Kwahani Marehemu Ahmada Yahya Abdulwakil yaliyofanyika Kijijini kwao Muyuni.
Akisoma Wasifu wa Marehemu Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Mjini Awadh Haji amesema Marehemu atakumbukwa kwa namna alivyokuwa akishirikiana na Viongozi wengine kuwaletea Wananchi Maendeleo.
Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Hamad Yussuf Masauni na Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera Uratibu na Baraza la Wawakilishi Hamza Hassan Juma wakatoa salamu za Serikali na kumueleza Marehemu kama Kiongozi wa Mfano katika kuihudumia Jamii.
Marehemu Ahmada Yahya Abdulwakil Amefariki na Kuacha Vizuka Wawili na Watoto 17.
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Peponi ,Amiin