Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa, amezindua nembo na kauli mbiu ya Miaka 60 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar huku akiwataka Watanzania kuutumia uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mwaka huu kuchagua Viongozi wenye nia njema na Muungano.
Mhe. Kassim Majaliwa, ameyasema hayo Jijini Dodoma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Nembo hiyo ambapo amewataka Watanzani kuulinda Muungano huo.
Majaliwa amewataka Watanzania wote, Bara na Visiwani kundelea kuulinda, kuuenzi, kujivunia na kuuthamini Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Mhe.Dkt. Selemani Jafo,amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt.Ali Hussein Mwinyi kwa kutatua hoja mbalimbali za Muungano.