Zanzibar Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewaongoza Maelfu ya Wazanzibar katika Dua maalum ya Hitma ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume.
Dua hiyo ilihudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, Dini pamoja Wananchi imefanyika katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar ikiwa ni Kumbukumbu ya Kifo cha Hayati Mzee Karume ambapo aliuawa Aprili 7,1972.
Mara baada ya kumalizika kwa Dua hiyo ya Hitma iliongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab Dk. Mwinyi aliwaongoza Viongozi na Familia ya Hayati Mzee Karume kwenye Kaburi la Mzee Karume na kuomba Dua na kuweka Mashada ya Maua.
Viongozi wa Madhehebu ya Dini mbali mbali walimuombea Dua Hayati Mzee Karume ambao ni Dini ya Waisalamu, Wakristo na Wahindu. katika Dua hiyo ilihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philipy Isidory Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa.
Wengine ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdullah, Makamu Mwenyekitiki wa CCM Bara Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Emanuel Nchimbi.
Wengine ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanzia Dk. Tulia Akson, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Mufti Mkuu wa Tanzania, Mufti Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mawaziri mbali mbali kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.