RIBA BOT YAPANDA SABABU MWENENDO WA UCHUMI WA DUNIA

RIPOTI BOT

   Benki Kuu ya Tanzania  BOT  imepandisha Riba kutoka Asilimia 5.5 iliyotumika  katika Robo ya Kwanza ya Mwaka hadi asilimia 6 ambayo itatumika katika Robo ya Pili ya Mwaka kuanzia Mwezi April hadi Juni 2024.

   Hayo yameelezwa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania BOT Emmanuel Tutuba wakati alipokuwa Akizungumza na Wadau wa Taasisi za Kibenki na Mitandao ya Simu Jijini Daes salaam amesema uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha Kamati ya Sera ya Fedha     ( MPC) kilicho fanyika April 3 2024 na kuzingatia Thamani ya mwenendo wa uchumi iliyofanyika Mwezi Marchi Mwaka huu.

    Amesema kutokana na thamani ya Mwenendo wa Uchumi wa Dunia katika Robo ya Kwanza ya Mwaka 2024 ukuaji wa uchumi umeimarika katika Nchi zinazoendelea na zile zinazoibuka kiuchumi na kwa upande wa Tanzania umeendelea kuimarika licha ya changamoto zinazotokana na mtiririko wa uchumi wa Dunia ambao unakadiriwa kufikia Asilimia 5.1. kwa Mwaka 2023.

   Akizungumzia mwenendo wa Uchumi kwa upande wa Zanzibar Gavana Tutuba amesema umeendelea kuwa wa kuridhisha ambapo unakadiriwa kukuwa kwa zaidi ya Asilimia 6 kwa Mwaka 2023 kutokana na kuimarika kwa Shughuli za kiuchumi ,Hususan Utalii.

     Amesema mfumuko wa Bei unaendelea kuwa tulivu kwa Wastani wa Asilimia 3.0 kwa Robo ya Kwanza ya Mwaka 2024 kiwango kicho kilikuwa ndani ya lengo la Nchi la mfumo wa bei usiozidi Asilimia 5 kwa vigezo vya Kikanda kwa Jumuiya ambazo Tanzania ni Mwanachama na kwa upande wa Akiba ya Fedha za Kigeni amesema imeendelea kuwa ya kutosha zaidi ya Dola za Marekani Bilioni

5.3Mwishoni mwa Mwezi Marchi 2024.

      Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Taasisi za Kibenki Tanzania Theobald Sabi alisema juu ya ongezeko hilo .

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.