Waziri wa Maji Nishati na Madini Mhe.Shaibu Hassan Kaduara amesema Serikali inathamini michango uliotolewa na aliekuwa Kamishna wa Kwanza wa Polisi Zanzibar Marehemu Eddington Herbert Kisasi katika harakati Mapinduzi ya Zanzibar na baada ya Mapindunzi.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Nishati na Madini Joseph Kilangi wakati akizungumza katika Ibada ya kumuombea Marehemu Eddington Herbert Kisasi iliyofanyika katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi 'b' Mkoa wa Mjini Magharibi.
Ameesema Serikali itaendelea na utaratibu wa kuwaenzi Waasisi wa Taifa na kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ambayo walijitolea na kuyapigania ili kuondokana na madhila yalikuwa wakifanyika kabla ya Mapinduzi
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polosi Jonas Mahanga amemuelezea Marehemu Eddington Herbert Kisasi ni Kiongozi alietoa mchango mkubwa kwa Jeshi la Polisi katika Uongozi wake kuanzia Mwaka 1964 Hadi 1976
Akitoa neno la Shukrani la Wanafamilia Emanuel Kisasi amesema Wanaishukuru Serikali kwa utaratibu walioiweka kwani unawapa Faraja ya kutambua mchango ulioutoa Mzee wao.