FIKRA NA FALSAFA ZA MAREHEMU KARUME KUENDELEZWA

Washiriki wa Kongamano

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussen Ali Mwinyi amewataka Wananchi kuzienzi na kuziendeleza  fikra na falsafa za kimaendeleo na kizalendo za Marehemu Mzee Abeid Amani Karume kwa maslahi ya Taifa.

     Akifungua Kongamano la 6 la Kumbukumbu ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar Marehemu Mzee Abeid Amani Karume  katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akisoma hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla  amesema Marehemu Mzee Karume alijenga upendo na umoja wa Kitaifa, misingi bora ya kiuchumi, kuleta haki na kupambana na dhuluma dhidi ya Wanyonge.

      Amesema kutimia Miaka 52 ya Kumbukumbu ya Mzee Karume ni vyema kujikumbusha misingi ya utendaji wenye kuacha alama katika maisha na mifumo mbalimbali katika Serikali kwa kuendeleza na kukuza uzalendo miongoni wa Watu. 

      Aidha Dk.Mwinyi amesema ni muhimu Jamii kukumbuka na kurejea katika misingi ya falsafa za uwazi, uadilifu, ushirikishwaji, amani, upendo na ubunifu na utendaji wenye kuimarisha maisha ya Wananchi.         

     Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Mhe.Hamza Hassan Juma amesema Kongamano hilo linatoa fursa kwa Wananchi hasa Vijana kuzifahamu fikra na Falsafa za Marehemu Mzee Karume pamoja na makubwa aliyofanya ikiwemo kuikomboa Zanzibar na Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.         

     Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  Ndg.Shadrack Sakai Mwakalila amesema ni muhimu kuangalia Maendeleo ya Zanzibar kwa maono ya Marehemu Mzee Karume wakati Serikali ikitumia dhana ya Ichumi wa Buluu.

    Katika Kongamano hilo Mhe.Hemed amekabidhi zawadi kwa Washidi mbalimbali wa Insha iliyoakisi maisha ya Marehemu Mzee Karume kutoka Skuli za Msingi na Sekondari za Zanzibar.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.