Mamlaka ya Maji Zanzibar 'ZAWA' imehimizwa kuchukua hatua madhubuti zitakayowawezesha Wananchi wa maeneo ya Mjini na Vijijini kupata huduma za Maji Safi Salama.
Wajumbe wa Kamati ya Ardhi Mawasiliano na Nishati ya Baraza la Wawakilishi chini ya Mwenyekiti wake Mhe.Yahya Rashid Abdallah wametoa mapendekezo hayo mara baaada ya kutembelea na kupokea Taarifa ya utekekelezaji wa mradi wa kulaza mabomba Unguja na Pemba.
Wamepongeza kuwepo Miradi inayolenga kuongeza hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji Safi na Salama Nchini na kuishauri Mamlaka hiyo kuendelea kuhamasisha uhifadhi wa vyanzo vya Maji pamoja na kuyaainisha Maeneo yote ya Umma yenye matatizo ya ukosefu wa Maji na kuyatafutia vyanzo vya kujitegemea ili kuhakikisha yanapata maji ya kutosha kwa wakati wote.
Naibu Waziri wa Maji Nishati na Madini Mhe.Zawadi Amour Nassor na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA Mhandisi Dkt.Salha Mohammed Kassim wamesema Wizara inaendelea kuchukua juhudi zaidi katika kusimamia na kuhakikisha huduma za Maji zinawafikia Wananchi kwa kuzingatia mahitaji.