SERIKALI YAENDELEA NA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

MAJAALIWA AWAASHA MWEGE WA UHURU

     Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuepuka matumizi ya Dawa za Kulevya kwani yanaharibu nguvu kazi ya Taifa hasa Vijana ambao wanategemewa kuongoza na kufanya shughuli za uzailishaji pamoja na kuharakisha maendeleo.

     Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli katika Sherehe za Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa zilizofanyika kitaifa katika Uwaja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro.

     Amesema kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu wa udhibiti wa biashara ya Dawa ya Kulevya imeendelea kuongeza kasi ya mapambano ili kukomesha Biashara hiyo Nchini.

     Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa amesema Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka huu utaendelea kuhimiza mapambano dhidi ya Rushwa, huku akitoa Wito kwa Watanzania kupambana na vitendo vya Rushwa.

      Kwa upande wake Waziri wa Habari, Vijana Utanaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe.Tabia Mwita Maulid, amesema Mbio za Mwenge wa Uhuru zimeendelea kudumisha Uhuru, amani mshikamano, uzalendo na umoja wa Kitaifa pamoja na kuchocheo Maendeleo ya Kijamii.

     Awali, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi amesema Mwenge wa Uhuru umekuwa ukiwaunganisha Watanzania,

      Mbio za Mwenge wa Uhuru Mwaka 2024 zinaenda sambamba na Maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibara, Mapinduzi Matufuku ya Zanzibar, pamjo na Miaka 60 Tangu kuanza kwa Mbio hizo.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.