MAANDALIZI YA UZINDUZI WA MBIO ZA MWENGE 2024 YAMEKAMILIKA

MH. TABIA MAULID MWITA

Waziri wa Habari, Vijana na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Tabia Maulid Mwita amesema Maandalizi ya Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2024 yamekamilika huku akiwataka Watanzania kushiriki katika Uzinduzi huo.

Waziri Tabia amatoa Kauli hiyo akiwa katika Uwanja wa Chuo cha ushiriki Moshi Mkoani Kilimanjaro Mara baada ya kukagua Maandalizi ambapo amesema Waziri Mkuu Kasim Majaliwa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Uzinduzi huo kwa Niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi.

Bi Fatma Hamad ni Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Vijana na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema yapo mafanikio mengi yanayopatika kutoka na mbio za Mwenge wa Uhuru huku akisisitiza kuwa Mwenge hauna Chama wala Dini.

Mkoa wa Kilimanjaro ndio utakuwa Mkoa wa kwanza kukimbiza Mwenge kwa 2024 ambapo Mkuu wa Mkoa huo Nurdin Babu amesema Mwenge utakimbizwa katika Halmashauri zote za Mkoa huo huku akisema hakuna mradi utakaokuwa na shida ndani ya Kilimanjaro.

Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa Mwaka 2024 zinatarajiwa kukimbizwa katika Mikoa 31 yenye Jumla ya Halmashauri 195 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.