Wafanya kazi wa Mdhibiti na Wakaguzi Wakuu wa Hesabu za Serikali Kisiwani Pemba wameshauriwa kufanyakazi kwa Mujibu wa Mkataba wa uwajiri wao ili kuepuka matatizo kwa Jamii na kwa MwenyeziMungu .
Ushaur huo umetolewa na Mratibu wa Ofisi ya Mufti Pemba Nd.said Ahmad Mohamed wakati alipokuwa akizungunza na Watendaji wa Taasisi hiyo huko katika Ukumbi wa Mkaguzi wa Hesabu za Serikali Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba ,katika hafla ya kuwaombea Dua waliokua Watumishi wa Taasisi hiyo pamoja na Viongozi Wakuu wa Serikali
Amesema kufanya kazi kwa mujibu wa Mkataba wa muajiri utasaidia kuleta maendeleo katka Taasisi hiyo na iwapo watakwenda kinyume na utaratibu uliowekwa itasababisha kutokea kwa matatizo mengi.
Kwa upande wake Naibu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Dkt said Khamis Juma amewataka Watendaji hao kuzidisha mashirikiano ili kila mmoja aweze kunufaika na Taasisi hiyo .
Akizungunza kwa niaba ya Wastafu waliotumikia Taasisi hiyo Nd. Khamis Rashid Suweed ameushukuru uwongozi wa Taasisi wa udhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali kwa kwa kuwa na mabadiliko kwa Jamii pamoja na Serikali