ZRA YAPELEKA FARAJA KWA WATU WENYE MAZINGIRA MAGUMU

ZRA

    Mamalaka ya Mapato Zanzibar ZRA, imesema itaendelea kusaidia Watu wenye mazingira magumu na wenye Ulemavu ili kujiona wanathamani ndani ya Jamii.

     Akizungumza mara baada ya kugawa sadaka kwa Familia 300 ikiwemo Watu wenye mazingira magumu, Watoto wenye Ulemavu na Watu wasiojiweza, huko Bumbwini na Jangombe,  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mamalaka hiyo, Profesa Hemed Rashid Hikman.

     Amesema endapo Wananchi watahamisika kulipa Kodi kwa wakati itasaidia Serikali kufikia azma yake ya kuwasaidia Watu wenye uhitaji na kuimarisha huduma za Maendeleo ya Nchini.

     Aidha amesema kuwa msaada huo unatokana na Kodi za Wananchi ambao wamechangia katika kudai Risiti za Elektroniki pale wanapofanya manunuzi ya bidhaa mbalimbali.

      Nae Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Zanzibar ZRA, Ndg.Yussuf Juma Mwenda, amesema lengo la kufika maeneo hayo ni kutoa shukurani kwa Wananchi wa Zanzibar kwa mchango wa kulipa Kodi  hali inayochangia kupata maendeleo zaidi.

     Nao waliopatiwa msaada huo wameishukuru ZRA kuwa kuwapa msaada huo na kuomba waendeelee na utaratibu huo.

msaada uliotolewa  ni Mchele, Mafuta ya kupikia, Sukari na Fedha Taslim.

Tags
stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.