Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini kuendelea kusoma Qurani Tukufu na kufuata maelekezo yake ili Jamii iweze kufanikiwa Duniani na Akhera.
Dk.mwinyi ametoa wito huo katika kilele cha tunzo za Kimataifa za Qur-an Tukufu zilizoandaliwa na Jumuiya ya kuhifadhisha Qur-ani Tanzania chini ya Uongozi wa Sheikh Othman Kaporo na kufanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Diamond Jubilee
Amesema Ustawi wa Jamii upo katika Kitabu Kitukufu cha Qur-ani kwa Kusoma, kufahamu maelekezo yake na kuyaishi ili kila mmoja afanikiwe Duniani na Akhera.
Aidha Dk.Mwinyi amesisistiza Jamii kuwa na mikakati madhubuti katika kusimamia maadili mema kwa Vijana ili kuwa Taifa lenye Ustawi bora.
Kilele cha Tunzo za Kimataifa za Qur-an Tukufu zinazoandaliwa na Jumuiya Kuhifadhisha Qur-ani Tanzania hushirikisha Washiriki Kumi na Sita kutoka Nchi mbalimbali Duniani.
Mshindi kwa Mwanzo katika Mashindano hayo kwa Kundi la Wakubwa kutoka Libya amepata Zawadi ya Dola za Kimarekani Elfu 5000/ na kwa Kundi la Watoto Wadogo wenye Umri wa Miaka Kumi hadi Kumi na Mbili alikuwa ni Huzaifa Munir kutoka Bangladesh amepata Dola Elfu 5000/. na Mshindi wa Adhana kutoka Magharibi ni Ilyas Wardi na Amepata Dola 1500/.